MHARIRI


Dr. Tengio Urrio.

Blog hii ya ‘Tulonge Juu ya Afya Zetu’  inasimamiwa na Dr. Tengio Urrio, Daktari mwenye uzoefu wa miaka mingi ya kufanya kazi kwenye huduma za afya Tanzania na kwenye nchi nyingine humu Afrika. Baada ya kusoma chuo cha Makerere Uganda, Harvard University USA na kwa mda mfupi chuo cha Udaktari Muhimbili Dar es Salaam, Dr. Tengio Urrio amekuwa Daktari wa Wilaya Bagamoyo, Kondoa na Kasulu na Daktari wa Mkoa wa Ruvuma. Amefanya kazi makao makuu ya Wizara ya Afya akiwa mkuu wa Kitengo cha Huduma za Mama, Watoto na Lishe. Amefanya kazi Kenya na Shirika la Aga Khan na Gambia Afrika Magharibi na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wanadamu (UNFPA).
Dr Tengio Urrio ni mwandishi wa kitabu cha hadithi cha ‘The Girl From Uganda’ kilichochapishwa na The East African Education Publishers-Kenya. Kwa miaka mingi ameandika mfululizo wa makala zinazohusu afya na magonjwa kwenye magazeti mengi nchini Tanzania ambayo ni pamoja na ‘The Sunday News, The Guardian, Tumaini Letu,  Tanzannia Daima na Nipashe’  Mfululizo wa makala za Tanzania Daima na Nipashe zinazozungumzia  hali nyingi za kiafya na hasa magonjwa sugu ya kisukari, saratani, shinikizo la damu (Hypertension),  kiharusi (Stroke) na matatizo yatokanayo na kunywa pombe zimesaidia katika kueneza elimu juu ya magonjwa haya kwa wananchi wa Tanzania na nje ya Tanzania.
Dr. Tengio Urrio ni mhariri wa Gazeti jipya la kila wiki la Tulonge ambalo linasifiwa kama gazeti kabambe la Kiswahili la mambo ya afya ya Mtu Binafsi, ya Jamii, ya Taifa na Ulimwengu. Hili ni gazeti la kwanza la lugha ya Kiswahili linalozungumzia kwa ufasaha juu ya afya zetu na kuwapa watu kuchangia kuandika makala fupi au refu kuhusu afya zao binafsi, za ndugu na marafiki.
Dr. Tengio Urrio ni msimazi wa blog hii ya  ‘Tulonge Juu Ya Afya Zetu’ na anapatikana kwa simu 0712 002188, e mail bahimokahumba@yahoo.com na P.O.Box 72321 Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment