Repoti za mtandao za tarehe 23 Mwezi Februari 2012 zinasema ‘Rais Chavez ana saratani inayohitaji kupasuliwa’
Raisi Hugo Chaves
|
Raisi Hugo Chavez wa Venezuela alikuwa amelazwa hospitalini huko Cuba ambapo walimgundua kuwa alikuwa na saratani. Walimpasua na kumtibu kwa kutumia mionzi na baadye alirejea kazini. Baadaye aliporudi tena kupimwa pale walipompasua saratani palionekana bado pana saratani. Repoti ya wakati huo ilisema kuwa Raisi Chavez atarudi huko Cuba hapa karibuni kupasuliwa tena na ameisharudi kufuatilia matibabu yake.
Raisi Chavez aliwaambia wananchi wake kuwa ataenda Cuba kwa ajili ya matibabu na wasitegemee kumwona huko nchini kwa wiki chache zijazo. Alisema kuwa pamoja na kuhitaji kupasuliwa atatibiwa kwa kutumia mionzi.
Daktari bingwa wa saratani Mkolumbia Dr. Carlos Castro alisema kuwa kama Chavez atahitaji kutibiwa kwa mionzi atahitaji kutibiwa kwa siku 10 kwa hiyo itakuwa lazima amteue msaidizi wake wakati akiwa Cuba kwa matibabu.
Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi huko Venezuela ambapo Chavez ambaye ameishatawala kwa miaka 13 anataka asimame tena aongezewe miaka 6 mingine.
Chavez mwaka huu wa 2012 ana umri wa miaka 57. Chaves amekataa kata kata uvumi uliokuwa unaenea kuwa alikuwa na saratani ambayoi ilikuwa imeishasambaa na kwa hiyo hawezi tena kazi yake ya Urais na hawezi kusimama tena kugombea Urais. Kama atashindwa kugombea, mshindani wake Henrique Capriles wa umri wa mika 39 ambaye sasa ni Gavana wa jimbo moja huko Venezuela huenda akashinda kwani inavyoonekana chama cha Chaves hakina mtu mwenye nguvu ya kuwashinda wapinzani.
Chavez alipoenda kutibiwa kwa mionzi aliamua kujinyoa kichwa chake ili kama mionzi ingenyofoa nywele zake basi dalili hiyo haingeonekana sana. Wakati repoti hii ikiandikwa nywele zake zilikuwa zinarudi kuota.
Akiwazungumzia wananchi wake kwa TV alisema, "Ningependa kuendelea kuishi. Nataka niishi na nyie wananchi wangu, niendelee kupigania maisha bora na nyie mpaka mwisho wa maisha haya yangu alionipa Mungu.”
Madaktari walisema kuwa habari hizi kuwa saratani aliyokuwa nayo imetokea pale pale ilipotolewa saratani, siyo habari nzuri kwa kuwa kama una saratani; baada ya matibabu umehisi umepona na saratani ikitokea pale pale ilipokuwa; siyo jambo zuri; ni jambo ambalo halina matumaini makubwa. Kama ikitokea pale pale ilipokuwa zamani ni dalili kuwa iliyokuwepo haikupona.
Tarehe 24 February 2012 Chaves alienda Cuba tena kupasuliwa na kutibiwa kwa mionzi. Baadaye mwishoni wa mwezi wa tatu alitokea kwenye TV akiwaambia wanancni wake kuwa alikuwa akiendelea vizuri
Msomaji unaona kuwa saratani ya Rais Chavez siyo tu inatishia maisha yake bali hata kazi zake za Urais. Kama una uzoefu wa jinsi saratani ilivyotishia uhai na maisha yako, ya ndugu, rafiki au mtu yeyote unayemfahamu tuandikie. Tukichapisha uzoefu wako hatutatambulisha jina, anwani au simu kwa kuwa yote haya ni siri yako na mhariri
Tuandikie mhariri, P.O.Box 72321 Dar es Salaam, bahimokahumba@yahoo.com na 0712002188 au andika kwa hapa chini.
No comments:
Post a Comment