Kuhusu hii Blog

Blog hii ni nafasi ya kila mtu kulonga juu ya chochote kinachohusu afya yake, afya ya familia, marafiki na wafanyakazi wenzake,  afya ya jamii yake, taifa lake na hata ya mataifa na ulimwengu. Tunatoa nafasi kwa kila mtu kulonga kwa mda mfupi na mda mrefu. Unaweza ukalonga juu ya mambo mengi yanayohusu afya. Kwa mfano tuandikie juu ya unavyoumwa, ulivyoumwa au ndugu yako, rafiki yako, mfanyakazi mwenzako  anavyoumwa alivyoumwa. Andika juu ya matibabu ya sasa na ya huko nyuma, urahisi na matatizoo ya kupata matibabu. Andika unavyoendelea au ndugu yako anvyoenelea na matibabu na shida anazozipata. Sifia na kosoa huduma za afya kwa ujumla na wale wanaozitoa na kuzisimamia. Blog hii itaandika blog za wasomaji wengine wanaotaka kuchangia kwa mfano juu ya wanavyougua magonjwa sugu ya UKIMWI, presha ya damu, Kisukari, Saratani, Ugonjwa wa Akili nakadhalika. Post/Matoleo mengine ni ya mataizo ya kumtunza mtoto au mtu mzima, juu ya ndoto, mimba na kulea watoto. Humu unaweza ukaandika chochote tu kinachohusu afya.
Kwa kuanzia blog hii tunaandika juu ya Magonjwa ya Kina Mama, Magonjwa ya Kina Baba, Magonjwa ya Wazee, Magonjwa ya Watoto, Ugonjwa wa Kisukari, Ugonjwa wa Presha,  Ugonjwa wa Saratani, Ugonjwa wa Siko Selli, Maambukizi ya VVU na Syndroma ya UKIMWI, Kujamiana, Maendeleo ya Mimba kila Wiki, Kutoa Mimba, Kutunga Mimba na Kuzaa, Ukatili wa Kijinsia (UWAKI) na Watu Wanaowapiga Wake Zao, Magonjwa Yanayoambukizwa Kwa Kujamiana (MYKK), Watu Wasio na Rangi ya Ngozi, Macho na Nywele yaani Walemavu wa Rangi ya Ngozi, Mgonjwa wa UKIMWI, Chati na Daktari; Muulize Maswali.
Wafadhili na Matangazo ya biashara
Blog hii inakaribisha wafadhili, matangazo ya biashara na ya huduma mbali mbali
Tuandikie

No comments:

Post a Comment