Ukiwa na swali mpelekee daktari meseji 0712002188 mtachati na atakuandikia jibu hapa na kwenye simu yako au anika kwa hapa chini.
Msomaji: Nina tabia ya kula udongo. Unajua ule udongo wanaouza sokoni kipande kikiuzwa shillingi hamsini. Tangu nianze kupata siku zangu za mwezi kuna miezi ambayo najisikia sana hamu ya kula udongo na hata huko kijijini kwetu tunakoishi kwenye nyumba isiyo na sakafu ya sementi nilikuwa nachimba udongo humo ndani ya nyumba na kuula. Baba na mama walikuwa wananigombeza eti nisile udongo na nisichimbe humo ndani ya nyumba lakini sikuweza kuwasikiliza kwani nilikuwa nasikia sana hamu ya kula idongo. Hamu hii inakuja sana wakati mvua ikinyesha. Nikisikia tu mvua ikinyesha, nasikia kama harufu nzuri inatoka kwenye udongo uliokandika nyumba yetu ya kienyeji. Hamu hii ya kula udongo naisikia sana siku chache kabla ya kupata siku zangu za mwezi na nikishaanza siku za mwezi basi hamu inaisha na naacha kula udongo mpaka siku chache baadaye ambapo hamu inarudi; naanza kula udongo mpaka siku za hedhi zitakapoaanza tena ambapo hamu inaisha na kurudi tena siku chache kabla ya siku za hedhi. Nilipokuwa na mimba hamu hii ya kula udongo ilikuwa kubwa kuliko kawaida na nilikuwa nala udongo wakati wote mpaka nilipojifungua. Je hii ni hali ya kawaida?
Daktari: Nafikiri nisikujibu; niachie wasomaji wakujibu. Kwanza tuulize kama kuna wasomaji wanao uzoefu na hali hii au wanajua mtu au ndugu aliye na uzoefu na hali hii yaani anakula udongo wakati akiwa na mimba au anakula udongo wakati mwingine. Hali ya kupenda kula udongo inaitwa kwa kitaalamu ‘pica’ na hutokea kwa baadhi ya kina mama wakati wa mimba. Tunaomba akina mama walio na uzoefu na kula udongo wakati wana mimba, wakati wo wote mwingine, wakati wa mzunguko wa hedhi nakadhalika watuandike na baadaye tutamjibu huyu ndugu. Tuandikie kwa mhariri, P.O.Box 72321 Dar es Salaam au bhimokahumba@yahoo.com au simu 0712002188
Nataka kuishi mda mrefu nifanyeje?
Acha Kuvuta Sigara
Kama unavuta sigara wacha sigara. Kutovuta sigara kunakuongezea mda wa kuishi hapa duniani, mda wa kuishi na afya nzuri. Ukivuta unajipunguzia miaka ya kuishi hapa duniani na mda wa kuishi ukiwa na afya nzuri.
Kweli? Unajuaje? Huko Ulaya kwa miaka 50 yaani nusu karne wamefanya utafiti wa kuwachunguza wavutaji na wasiovuta. Wamewafuatilia watu ambao wamevuta sigara na kurepoti wamevuta kwa miaka mingapi na waliovuta wamekufa wakiwa na miaka mingapi. Waliovuta na kuacha mapema waliishi mda mrefu kuliko walioacha wamechelewa. Kwa mfano walioacha wakiwa na umri wa miaka 30 waliongeza mda wa kuishi kwa miaka 10; walioacha wakiwa na miaka 40 walijiongezea mda wa kuishi kwa miaka 9, walioacha wamefikia miaka 50 walijiongezea mda wa kuishi kwa miaka 6, walioacha wakiwa na mika 60 walijiiongezea mda wa kuishi kwa miaka 3. Si unaona kuwa ukiacha mapema utajiongezea mda wa kuishi kwa miaka mingi zaidi kuliko ukiacha umechelewa, umezeeka? Acha sasa kama unavuta na kama hujaanza kuvuta, usianze
Haya masigara yanafupisha maisha
|
Tuandikie mhariri, P.O.Box 72321 Dar es Saaamu au bahimokahumba@yahoo.com 0712002188 tueleze una umri wa miaka mingapi, umeishavuta kwa miaka mingapi, unavuta sigara ngapi kwa siku. Ukiacha sasa utajiongezea mda wako wa kuishi kwa miaka mingapi? Ukiendelea utakufa mapema kwa miaka mingapi? Wiki ijayo kwenye kuishi mda mrefu tutaandika, “Ili uishi mda mrefu-funga ndoa; olewa kwa mwanamme umpendaye; akupendaye, oa mwanamke umpendaye; akupendaye”
Swali la kijanja/Swali la papo kwa papo
Taja saratani mbili zinazozuilika kwa kutoa chanjo. Tupelee jibu kwa sms 0712002188
Ukiwa mtoto wa sekondari taja umri na unasoma wapi, fomu gani ili ukipata jibu sahihi upelekewe zawadi.
HABARI yako doctor,pole na kazi....plz nataka kupata mtoto na umri wangu unakwenda nimesha zunguka sana kutafuta uzazi lakini sijafanikiwa.naomba ushauri wako nifanye nini?
ReplyDelete