Kubalehe ni ule muda ambao mtoto wa kiume na wa kike anabadilika mwilini akielekea kuwa mwanadamu mwenye uwezo wa kuzaa.
Muda wa kubalehe ni muda ambao kunakuwa na mabadiliko kwenye mwili wa msichana au mvulana kumfanya awe mwanadamu mwenye uwezo wa kuzaa. Muda wa kubalehe yaani muda wa mabadiliko kwenye mwili wa msichana na mvulana ili kumfanya awe na uwezo wa kuzaa, huanza mapema kwa wasichana wakiwa na umri wa miaka kama kumi na kuisha wakiwa na miaka kama 14 mpaka 16. Wavulana huchelewa kidogo na huanza miaka 12 na kuisha wakifikia miaka 18. Haya ni makisio tu ya miaka maana huenda kubalehe kukaanza mapema zaidi na kuchelewa kuisha.
Kwa wasichana dalili kuwa wapo kwenye huu umri wa kubalehe, maziwa yanaanza kuwa makubwa, nywele zinaota sehemu za siri na kwenye makwapa; wanakuwa na chunusi na baadaye wanavunja ungo yaani wanapata damu ya mwezi ya kwanza. Wavulana wanaota nywele vile kwenye sehemu za siri na kwenye makwapa, wanaota ndevu, viungo vyao vya kiume yaani korodani na uume vinakua, musuli inakuwa mikubwa na sauti inakuwa nzito.
Wakati wa kubalehe vile vile ni wakati wa kuongeza kasi ya kukua haraka haraka na kurefuka. Wanakua haraka kwa miaka kama mitatu hivyo baada ya kubalehe wanakuwa wameishafikisha karibu na urefu wao wa utu uzima.
Msichana anayebalehe
|
Wakati wa kubalehe mtoto anajisikia kuwa angependa kuwa na uhuru zaidi, hujiangalia zaidi kimwili akiona jinsi anavyobadilika, huangalia mavazi anayovaa kujiweka katika hali ya kwenda na wakati na mavazi wanayovaa wenzake wa umri huo, wanaweza zaidi kuwasikiliza vijana wakubwa na hata kukopi tabia, matendo na mavazi yao.
watoto ambao hawajabalehe
|
Pamoja na kukopi, kuwasikiliza na kuwadodosa wakubwa zao, wakati wa kubalehe mtoto anaendeleza uwezo na kipaji chake cha kutambua mema na mabaya. Ni wakati ambao mtoto anahitaji ukaribu na misaada ya wazazi na ya wale anaoishi karibu naye kumwezesha kujenga tabia nzuri ya kumsaidia maishani na katika utu uzima.
Tunakaribisha maswali na mawazo kuhusu kubalehe kutoka kwa vijana na wazazi. Mwandikie Mhariri bahimokahumba@yahoo.com 0712002188 au andika hapa chini.
No comments:
Post a Comment